Wakati ule wa utumwa wa wana wa Israel nchini Misiri Mungu alimsaidia Yusufu kufasiri ndoto ya Farao, ni ndoto hii na fasiri yake sahihi ndizo zilisaidia nchi ya Misiri kuwa taifa lenye nguvu kuliko mengine ya wakati wake {Mwanzo 41}. Baada ya tafsiri ya ndoto ile Farao alimteua Yusufu kuwa mtendaji wake mkuu ili kufanikisha fasiri ya ndoto yake (Farao) na kupitia Yusufu Misiri ilitumia vyema miaka saba ya neema kujikusanyia nafaka ya kuwatosha wao na mataifa ya jirani katika miaka saba ya ukame na dhiki, si tu taifa la Misiri lilipata chakula bali pia liliweza kuwa na nguvu kuliko yote kwa sababu ya utajiri uliotokana na hekima ya Yusufu.
Ninapoyatazama matukio ya Somalia na ukosefu mkubwa wa chakula nayafananisha na ndoto ya mtumwa Yusufu nchini Misiri, njaa ya aina hii haitakuwa ya mwisho, historia inatuambia kuwa angalau kila baada ya miaka kumi kunakuwa na ukosefu mkubwa wa chakula unaotokana na ukame. Kwa kutumia ukweli huu naona hii ni baraka kwani tukiitumia vizuri itakuwa ni fursa ya kutuwezesha kufaidika na ukosefu mkubwa wa chakula wa mwaka 2021 kama ambavyo Misiri iliweza kujikusanyia chakula kwa kipindi cha miaka ile saba ya neema.
Tatizo kubwa la uzalishaji nchini kwetu ni ukosefu wa maji, lakini bahati nzuri ni kwamba mvua hunyesha na mtu akichimba bwawa anauhakika wa kuwa na maji ya kutosha ndani ya miaka mitatu.
Ushauri wangu:
Tuanze sasa kujiandaa na ukame wa 2021 kwa uzalishaji wa chakula cha ziada tukiweka mkazo kwenye kilimo cha umwagiliaji, bahati nyingine nzuri ni kuwa sasa kuna fursa nyingi ambazo zinasubiri kuchukuliwa. Nitatoa mfano wa pesa zinazotarajia kutolewa na wahisani kupitia mradi wa SAGCOT (google neno hili kwa taarifa zaidi). Lakini bila maandalizi sasa fursa hizi zitachukuliwa na wageni na tutaendelea kulalamika bila mambo kubadilika sana.
Kijijini kwetu kuna jamaa alikuwa anachimba malambo kwa ajiri ya kunyweshea mifugo na gharama yake siyo kubwa sana, mimi nitafanya majaribio kwa kuchimba bwawa kutumia mheshimiwa huyu. Lakini kitu kingine ambacho tunaweza kuanza kujiandaa ni kujikusanya ili tuwe na nguvu ya pamoja na tuweze kunufaika na fedha zinazotolewa kupitia madirisha kama hili la SAGCOT ambalo linaweka msisitizo zaidi katika kuwaendeleza wakulima wadogo kupitia vikundi vyao, lakini pia ili umoja una manufaa mengine kuwa uzalisha unapokuwa mkubwa inakuwa rahisi kupata soko na pia kuweza kuongeza thamani kwa urahisi.
Pia msisahau kuchangamkia fursa ya kupata ardhi, nasiki Lindi kuna maeneo mengi ya wazi ambayo tunaweza kuyachangamkia na kujinufaisha kama wawekezaji wa ndani, nitakuwa na safari ya ya kuuelewa mkoa wa Lindi mwezi August nakaribisha kwa yeyote atakayependa tufanye safari hii pamoja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mimi naungana nawe kwenye safari ya kwenda Lindi kutafuta Ardhi.
ReplyDeleteChangamoto iliyopo, ni kuwa sie wawekezaji wadogo kuja kutambuliwa na SAGCOT (Southern Africa Growth Corindor of Tanzania), Makampuni kama TATEPA, ....,n.k ndio yanaweza kufaidi miradi hiyo au Window hiyo ya kilimo.
Tutajaribu, ila najua mambo si malahisi.